Orhan Pamuk
From Wikipedia
Ferit Orhan Pamuk (amezaliwa 7 Juni, 1952) ni mwandishi kutoka nchi ya Uturuki. Katika hadithi zake anajaribu kuunganisha riwaya ya Ulaya ya kisasa na mapokezi ya nchi za Mashariki. Mwaka wa 2006 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.