Patrice Lumumba
From Wikipedia
Patrice Lumumba (2 Julai 1925 – 17 Januari 1961) alikuwa mwanasiasa mwanamapinduzi wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mwaka wa 1958 alikuwa miongoni mwa waanzishaji wa Chama cha Taifa la Kongo (kwa Kifaransa: Mouvement National Congolais). Mwaka wa 1960 alipata kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuongoza harakati za kugombea uhuru toka kwa utawala wa kikoloni wa Wabelgiji. Baada ya miezi kumi tu ya kuwa Waziri Mkuu, Lumumba alipinduliwa na baadaye kutiwa ndani kabla ya kuuawa katika mazingira ya kutatanisha katika eneo la Katanga upande wa kusini wa Kongo.
[edit] Filamu
[edit] Viungo vya nje
Taarifa mbalimbali kuhusu Lumumba
- Msamaha wa mauaji ya Lumumba
- Matangazo ya BBC siku ya kifo cha Lumumba
- Matokeo ya uchunguzi wa Tume ya Ubelgiji
- Historia ya Lumumba
- Mauaji ya Lumumba