Port Louis
From Wikipedia
Port Louis ni mji mkuu wa jamhuri ya Morisi. Ikiwa na wakazi 170,000 ni mji mkubwa wa taifa hili la visiwani katika Bahari Hindi.
Kiwanja cha kimataifa cha ndege cha Sir Seewoosagur Ramgoolam kipo 30 km kusini ya mji. Kutoka Port Louis kuna feri kwenda Saint Denis mji mkuu wa Réunion.
Kuna viwanda vya nguo na vitambaa pia vya kemikali na madawa. Benki ziko nyingi. Kwa jumla Port Louis ni mji wa Afrika ambako wenyeji wana hali ya maisha iliyo juu kushinda miji mingine ya Afrika.