Rasi ya Sinai
From Wikipedia
Rasi ya Sinai (Kiar.: sina' سيناء) ni rasi yenye umbo la pembetatu nchini Misri upande wa kaskazini ya Bahari ya Shamu inayounganisha bara za Afrika na Asia. Inahesabiwa kuwa sehemu ya mwisho wa Asia ya Magharibi.
Eneo la Sinai ni takriban 60,000 km² hasa jangwa. Imepakana na Ghuba ya Suez upande wa magharibi na Ghuba ya Aqaba upande wa mashariki. Upande wa magharibi Mfereji wa Suez unaunganisha Bahari ya Shamu na Mediteranea. Kaskazini ya mwisho wa Ghuba ya Aqaba ni mpaka kati ya Misri na Israel.
Mahali panapojulikana zaidi ndani ya eneo al rasi ni mlima Sinai (pia: mlima Horeb, jabal Musa) unaoaminiwa ni mahali ambako Musa alipokea amri kumi za Mungu.
Kwenye pwani la rasi utalii ni sehemu muhimu ya uchumi.