Barafuto
From Wikipedia

Barafuto huitwa pia "mto wa barafu". Ni kanda kubwa la barafu iliyoanza kutambaa kutokana na uzito wake ikifuata uvutano kwenye mtelemko. Kwa sababu hiyo barafuto zinapatikana hasa mlimani.
[edit] Asili ya barafu ya barafuto
Barafuto zimetokana na theluji inayokaa miaka mingi bila kuyeyuka katika mazingira baridi. Theluji mpya inakaa juu ya theluji ya miaka iliyotangulia. Uzito wa theluji ya baadaye inakandamiza ile ya chini. Kutokana na shindikizo hili theluji ya chini hubadilika kuwa barafu kabisa.

Barafuto ni kati ya nguvu kubwa za mmomonyoko duniani.
Afrika ina barafuto ndogo kadhaa juu ya mlima Kilimanjaro na mlima Kenya lakini zinaelekea kupotea kutokana na uhaba wa mvua itakayobadilika kuwa theluji mpya.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Barafuto" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Barafuto kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |