Charles Richet
From Wikipedia
Charles Robert Richet (25 Agosti, 1850 – 4 Novemba, 1935) alikuwa daktari na mwanafiziolojia kutoka nchi ya Ufaransa. Hasa alichunguza vimiminiko vya mwili kama damu, jasho na kadhalika. Mwaka wa 1913 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.