Dola-mji
From Wikipedia
Dola-mji ni dola ambalo eneo lake ni mji mmoja pekee.
Katika historia kuna mifano mingi ya dola-miji. Sasa (mnamo mwaka 2006) kuna mitatu pekee ambayo ni dola-miji ya kujitegemea kabisa. Pamaja nayo kuna pia madola au majimbo ndani ya shirikisho yanayoweza kuitwa "dola-mji".
Contents |
[edit] Dola-mji wa kujitegemea kabisa
Dola-mji wa kujitegemea kabisa ni:
Wakati mwingi Kuwait huitwa pia "Dola-mji" kwa sababu karibu wakazi wote wa dola huishi katika mazingira ya Kuwait mjini. Lakini kuna miji midogo mingine nchini.
[edit] Dola mji kama jimbo la kujitawala ndani ya shirikisho
Dola mji kama jimbo la kujitawala ndani ya shirikisho ni kama mfano:
- Hamburg, Berlin na Bremen katika Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani
- Vienna katika Shirikisho la Jamhuri ya Austria
- Moscow na Sankt Petersburg ndani ya shirikisho la Urusi,
- Addis Ababa na Dire Dawa ambayo ni miji ya kujitawala (astedader akababiwach) katika Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia
- Ceuta na Melilla ambayo ni miji ya kujitawala (ciudades autónomas) ya Hispania
Uchina si shirikisho lakini miji ya Hongkong na Makau ina madaraka makubwa ya kujitawala nje ya sheria za Uchina bara.
[edit] Dola-miji katika historia
Dola miji ilikuwa muhimu sana katika nchi nyingi kihistoria. Hasa wakati katika nchi fulani hakuna serikali ya juu miji ilijitawala kabisa na kushindana na miji mingine na falme.
[edit] Dola-miji katika karne ya 20
Karne ya 20 ilikuwa na dola-miiji kadhaa hasa kati ya vita kuu ya kwanza na ya pili.
- Fiume (Rijeka) katika Kroatia ya leo
- Trieste katika Italia ya leo
- Danzig (Gdansk) katika Poland ya leo
- Memel (Klaipeda) katika Lithuania ya leo
[edit] Dola-miji ya zamani
- Miji ya Waswahili kwenye pwani la Afrika ya Mashariki ilikuwa dola-miji ya kujitegemea kama vile Mombasa, Malindi, Lamu, Pate na Kilwa. Wakati mwingine utawala wao ulienea zaidi, lakini kimsingi ilikuwa kila mji unaotawala eneo lake.
- Miji ya Uarabuni ilijitegemea kabisa kwa muda mrefu, kwa mfano Maka na Madina
- Ugiriki ya Kale ilikuwa na dola-miji mingi. Athens, Sparta, Korintho zilikuwa kwa muda mrefu miji tu pamoja na vijiji vichache. Zilijaribu kupanuka hasa Athens ilifaulu.
- Katika Italia ya nyakati za kati miji muhimu ilijitawala kabisa. Kati ya dola-miji iliyoweza kupanua eneo lao ni hasa Genova na Venesia.
- Dola la Ujerumani lilikuwa na dola-miji mingi hadi karne ya 19. Iliyobaki hadi leo na hali ya pekee ndani ya shirikisho la jamhuri ni Hamburg na Bremen. Mji wa Berlin ambao leo ni jimbo la kujitegema haukuwa dola-mji katika historia.
[edit] Links
Categories: Dola-Mji | Miji | Nchi | Nchi ndogo sana