Hispania
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Plus Ultra (Kilatini kwa "Mbele na zaidi") |
|||||
Wimbo wa taifa: Marcha Real au Marcha Granadera | |||||
Mji mkuu | Madrid |
||||
Mji mkubwa nchini | Madrid | ||||
Lugha rasmi | Kihispania(1) | ||||
Serikali
Mfalme
Waziri Mkuu |
Ufalme wa kikatiba Juan Carlos I José Luis Rodríguez Zapatero |
||||
Kuungana kwa nchi Kungana kwa ndoa za wafalme Maungano Hali halisi Kisheria |
1516 1716 1812 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
504,782 km² (ya 50) 1.04% |
||||
Idadi ya watu - Januari 2006 (kadirio rasmi) kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
44.395.286 (ya 29) 40,847,371 87.8/km² (ya 106) |
||||
Fedha | Euro (€)(2) (EUR ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CETTemplate:Fn (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
Intaneti TLD | .es | ||||
Kodi ya simu | +34 |
||||
Template:Fnb Majimbo ya kujitawala ya Hispania yanatumia lugha za: Kikatalan/Kivalencia, Kibaski na Kigalicia pamoja na Kihispania. Katika Bonde la Val d'Aran lahaja ya Kiarani ya lugha ya Kioksitani ni lugha rasmi pamoja na Kihispania; Template:Fnb Hadi 1999: Peseta Template:Fnb Ispokuwa Visiwa vya Kanari |
Hispania ni nchi ya Ulaya ya kusini-magharibi. Imepakana na Ufaransa, Andorra, Ureno na eneo la Kiingereza la Gibraltar. Kuna pwani ndefu ya Bahari ya Mediteranea na pia ya Atlantiki. Visiwa vya Baleari kwenye Mediteranea na Visiwa vya Kanari katika Atlantiki pamoja na miji ya Afrika ya Kaskazini Ceuta na Melilla ni sehemu za Hispania.
Mji mkuu ni Madrid ambayo ni pia mji mkubwa wa nchi. Eneo la nchi ni 500,000 km² kuna wakazi milioni 40.
Lugha rasmi ni Kihispania lakini majimbo 17 yamepewa ya kujitawala katika mambo mbalimbali pamoja na siasa ya kiutamaduni hivyo lugha za Kikatalan, Kivalencia, Kibaski na Kigalicia zimekuwa lugha rasmi za kijimbo pamoja na Kihispania.
Wahispania walio wengi ni wafuasi wa kanisa Katoliki.
Muundo wa serikali ni Ufalme wa Kikatiba. Mfalme Juan Carlos I amevaa taji tangu mwaka 1978. Anaheshimiwa sana kwa sababu aliongoza taifa katika mabadiliko ya kutoka katika udikteta wa jenerali Francisco Franco kuelekea demokrasia. Hasa tendo la mfalme la kuzuia mapinduzi wa kijeshi linakumbukwa sana. Lakini kisheria madaraka yake ni madogo.
Utawala uko mkononi mwa serikali inayochaguliwa na bunge. Bunge laitwa "Las Cortes likichaguliwa katika kura ya kidemokrasia.
Contents |
[edit] Historia
[edit] Historia ya kwanza
Wakazi wa kwanza waliojulikana kwa jina kuwa waliishi Hispania walikuwa Wakelti. Katika karne za kwanza KK Wafinisia walianzisha miji na kuchimba madini hasa shaba na fedha.
[edit] Waroma
Waroma wa Kale walivamia na kutawala Hispania kwa karne wakileta lugha yao ya Kilatini kilichokuwa msingi wa lugha za kisasa za Hispania. Kibaski pekee si lugha ya Kirumi.
Katika karne ya tano makabila ya Kigermanik walivamia Dola la Roma pamoja na Hispania. Wavandali na Wavisigothi walitawala juu ya sehemu kubwa ya Hispania.
[edit] Waarabu
Tangu mwaka 711 jeshi la Waarabu Waislamu liliingia kutoka Afrika ya Kaskazini na kutwaa sehemu kubwa za Hispania. Walipanuka karibu hadi milima ya Pirenei lakini watawala wa maeneo kadhaa katika kaskazini walijitetea na kufaulu kushika uhuru wao. Waarabu walileta fani nyingi za maendeleo nchini.
Katika kipindi cha vita za karne nyingi Wakristo wa Kaskazini walifaulu polepole kuwarudisha Waarabu hadi kusini ya nchi. Mwaka 1492 mfalme Boabdil wa Grenada mji wa mwisho wa Waarabu alishindwa na mfalme Ferdinand II wa Aragon na malkia Isabella wa Kastilia.
[edit] Koloni za Amerika
Wiki chache kabla ya kushinda huko Granada wafalme wa Hispania walimkubali nahodha Kristoforo Kolumbus na kumpa kibali cha kutafuta njia ya kufika Bara Hindi. Badala ya kufika India Kolumbus alifika kwenye visiwa vya Amerika ya Kati.
Hii ilikuwa mwanzo wa upanuzi wa Hispania katika "Dunia Mpya" ya Amerika. Wahispania walijenga dola kubwa ya kikoloni na kutwaa karibu Amerika ya Kusini yote pamoja na Amerika ya Kati na Mexiko hadi sehemu za kusini za Marekani ya leo.
Katika miaka mia tatu iliyofuata Hispania ilitajirika sana kutoka utajiri wa Amerika.
(ya kuendelea)
[edit] Miji mikubwa
- Madrid ni mji mkuu - wakazi 3,200,000.
- Barcelona - wakazi 1,600,000
- Valencia - wakazi 800,000.
- Seville - wakazi 705,000.
- Zaragoza katika Aragon- wakazi 650,000.
- Malaga katika Andalucia - wakazi 560,000.
- Murcia katika bonde la Segura - wakazi 410,000.
- Las Palmas de Gran Canaria ni mji mkuu wa Visiwa vya Kanari - wakazi 378,000.
- Palma de Mallorca kwenye Visiwa vya Baleari - wakazi 375,000.
- Bilbao ya Ubaski katika kaskazini - wakazi 350,000.
[edit] Picha za Hispania
Nchi na maeneo ya Ulaya | |||
---|---|---|---|
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Eire | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Italia | Jamhuri ya Masedonia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Malta | Moldova | Monako |Montenegro | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikani
Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1 Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini2 Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro
|