Vienna
From Wikipedia
Vienna (Kijer.: Wien) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Austria. Iko katika mashariki ya Austria kando la mto Danubi. Idadi ya wakazi imezidi milioni moja na lakhi sita. Vienna ina cheo cha jimbo ndani ya shirikisho la jamhuri ya Austria.
[edit] Utawala
Vienna imegawiwa katika mitaa 23.
|
[edit] Utamaduni
Kwa karne nyingi Vienna ilikuwa mji mkuu wa dola kubwa. Wafalme na makaisari wa familia ya Habsburg walitawala Dola Takatifu ya Kiroma hadi 1806 na baadaye na maeneo makubwa ya Ulaya ya kusini-mashariki hadi 1918. Hivyo Vienna ina majengo mazuri inayotunza kumbukumbu ya enzi za kale sio tu mji mkuu wa Austria ndogo ya leo.
Watu wa Vienna hukumbuka wasanii walioishi katika mji wao kama watunga muziki Wolfgang Amadeus Mozart, Ludwig van Beethoven na Brahms.
[edit] Viungo vya Nje
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Vienna" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Vienna kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |