Florini
From Wikipedia
Florini ni dutu sahili na halojeni simetali. Namba atomia yake ni 9. Katika mazingira yetu kawaida iko katika hali ya gesi yenye rangi njanokijani. Alama yake ya kikemia ni F.
Kwa kawaida hupatikana kama molekuli ya F2. Kati ya elementi zote mmenyuko wake wa oksidisho ni kali sana. Tabia hii inasababisha Florini kuwa sumu kali. Inamenyuka vikali na karibu elementi zote.
Makala hiyo kuhusu "Florini" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Florini kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |