Kengewa
From Wikipedia
Kengewa | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Kengewa
|
||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Kengewa ni ndege mbua wa jenasi mbalimbali (angalia sanduku ya uainishaji) ya familia Accipitridae. Wana mabawa marefu na mwika mrefu mwenye miraba myeusi na myeupe. Kengewa mlanyuki na kengewa wa Asia hula nyuki, nyigu na asali hasa lakini spishi zingine hula wanyama wadogo. Hujenga tago lao juu ya mti msituni.
Mpaka juzi kengewa mlanyuki tu ameonwa Afrika kusini kwa Sahara, lakini mwaka 2005 kengewa wa Asia ameonwa huko Gaboni.
[edit] Spishi za Afrika
- Pernis apivorus, Kengewa Mlanyuki (European Honey Buzzard)
- Pernis ptilorhynchus, Kengewa wa Asia (Oriental Honey Buzzard)
[edit] Spishi za mabara mengine
- Chondrohierax uncinatus (Hook-billed Kite)
- Henicopernis infuscatus (Black Honey Buzzard)
- Henicopernis longicauda (Long-tailed Honey Buzzard)
- Leptodon cayanensis (Grey-headed Kite)
- Leptodon forbesi (White-collared Kite)
- Pernis celebensis (Barred Honey-buzzard)