Manama
From Wikipedia
Manama ni mji mkuu wa Bahrain pia mji mkubwa wa nchi mwenye wakazi 150.000. Iko katika kaskazini ya nchi ambako kuna ardhi yenye rutba kiasi tofauti na jangwa tupu katika kusini.
[edit] Historia
Manama imejulikana tangu karne ya 14 ilipotajwa katika maandiko. Ilitawaliwa na Ureno katii ya 1521 hadi 1602, na Uajemi kati ya 1602 hadi 1783. Baadaye imekuwa makao ya familia ya kifalme ya Al-Khalifa inayotawala nchi. Tangu 1971 imekuwa mji mkuu wa Bahrain.