Mapigano ya Tours na Poitiers
From Wikipedia
Mapigano ya Tours na Poitiers ilikuwa vita ya mwaka 732 kati ya jeshi la Waarabu Waislamu kutoka Hispania na jeshi la Wafranki katika Ufaransa ya Kati.
[edit] Waarabu katika Ulaya
Waarabu walikuwa walienea katika sehemu kubwa ya Hispania tangu mwaka 711 wakaendelea kushambulia maeneo ya Wakristo katika Kaskazini. Jeshi la mwaka 732 likiongozwa na jemadari Abdul Rahman Al Ghafiqi lilivamia miji ya Ufaransa na kubeba mateka yao.
[edit] Mapigano
Jeshi la Wafranki (kabila kubwa ya Wagermanik waliotawala Ufaransa) chini ya makamu wa kifalme Karolo Martell lilikutana nao karibu na miji ya Tours na Poitiers. Karolo aliwasubiri wanajeshi wa nyongeza kutoka kwa Waskasonia na Walangobardia, Waarabu waliwasubiri Wafranki watoke nje ya misitu walipokuwa na kambi yao. Mwishowe Waarabu walishambulia siku ya saba lakini walishindwa kuvunja msimamo wa Wakristo. Jemadari Abdul Rahman Al Ghafiqi aliuawa mapiganoni jeshi lake likakimbia na kurudi Hispania.
[edit] Umuhimu kwa historia ya Ulaya na ya Uislamu
Ushindi huu wa Wafranki hutazamiwa mara nyingi kama hatua muhimu ya kuzuia uenezaji wa Uislamu katika Ulaya ya Magharibi. Hata kama Waarabu walirudi miaka mitatu baadaye walishindwa tena wakikutana tena na Wafranki waliojiamini wakishikamana kuzuia majaribio yote ya Waarabu kueneza utawala wao nje ya Hispania.
Waarabu waliendelea kukaa Hispania kwa karne zilizofuata lakini uenezaji wao ulisimamishwa.Luokka:Taistelut