Shirikisho la Mikronesia
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Patriots of Micronesia | |||||
Mji mkuu | Palikir |
||||
Mji mkubwa nchini | Weno | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza (kitaifa), Kiulithi, Kiwoleaia, Kiyap, Kipohnpeia, Kikosraea, and Kichuuk (kijimbo) | ||||
Serikali | Jamhuri Joseph J. Urusemal |
||||
Uhuru Tarehe |
3 Novemba 1986 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
702 km² (ya 188) |
||||
Idadi ya watu - Julai 2006 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
108,500 (ya 192) 107,000 154/km² (ya 66) |
||||
Fedha | US Dollar (USD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+10) (UTC-) |
||||
Intaneti TLD | .fm | ||||
Kodi ya simu | +691 |
Shirikisho la Mikronesia ni nchi ya visiwani katika Pasifiki kaskazini ya Papua Guinea Mpya. Ni nchi huru inayoshirikiana na Marekani. Nchi ilikuwa eneo lindwa chini ya Marekani kwa niaba ya Umoja wa Mataifa ikapata uhuru wake 1986.
Contents |
[edit] Jiografia
Shirikisho lajumlisha sehemu kubwa ya funguvisiwa ya Karolini katika Mikronesia kanda la Pasifiki. Nchi ina majimbo manne ya kujitawala ambayo ni Chuuk, Kosrae Pohnpei na Yap. Visiwa vya Palau ni pia sehemu ya Karolini lakini ni nchi ya pekee.
Mji mkubwa wa nchi ni Weno (wakazi 17,624) kisiwani Chuuk lakini mji mkuu ni Palikir kwenye kisiwa cha Pohnpei.
[edit] Majimbo ya shirikisho
Kuna majimbo manne kama yafuatayo:
Bendera | Jimbo | Mji Mkuu | Eneo la nchi kavu[1] | Wakazi[2] | Msongamano |
---|---|---|---|---|---|
Chuuk | Weno | 127 km2 | 53,595 | 1,088 per km2 | |
Kosrae | Tofol | 110 km2 | 7,686 | 70 per km2 | |
Pohnpei | Palikir | 346 km2 | 34,486 | 100 per km2 | |
Yap | Colonia | 118 km2 | 11,241 | 95 per km2 |
[edit] Historia
Visiwa vimekaliwa na watu tangu miaka 4,000 hasa kutoka Rasi ya Malay na visiwa vya Indonesia. Wengine wametokea kutoka visiwa vya Polynesia.
Kisiwani Yap kulitokea dola na uatawala wa kifalme. Tangu kufika kwa Wahispania katika karne ya 16 visiwa vilikuwa chini ya ubwana wa nje lakini maisha ya kawaida yaliendelea bila mabadiliko makubwa kwa muda mrefu. Mwisho wa karne ya 19 Hispania iliuza koloni kwa Ujerumani; utawala wa Kijerumani ulikwisha katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ukachukuliwa na Japani hadi mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. JApani ilifuatwa na Marekani iliyoendelea kutawala kwa niaba ya UM hadi uhuru.
[edit] Uchumi
Uchumi wa nchi hutegemea hasa kilimo cha kujisukuma na uvuwi. Mapato ya serikali ni kutokana na vibali kwa wavuwi wa nje wanaovua samaki ndani ya maji ya shirikisho. Kuna pia uchimbaji wa fosfeti.
Hata hivyo shirikisho la Mikronesia pamoja na Nauru vina idadi kubwa la watu wanene duniani.