Sikukuu
From Wikipedia
Sikukuu ni siku maalumu ya kukumbuka, kusheherekea au kufurahika jambo fulani.
Kuna sikukuu za binafsi na sikuu za umma. Sikukuu ya umma mara nyingi huwekwa wakfu kisheria maana yake si siku ya kazi bali ya mapumziko.
Kati ya sikuu za umma kuna sikukuu za kidini na sikukuu za kiserikali.
Kati ya sikukuu za binafsi kuna siku za kukumbuka matukio ya pekee kama tarehe ya kuzaliwa, kumbukumbu ya siku ya kufunga ndoa na mengine.
Contents |
[edit] Sikukuu za Kidini
[edit] Sikukuu za kikristo
- Majilio
- Krismasi (Kuzaliwa kwake Yesu)
- Epifania
- Ijumaa Kuu (Kifo cha Yesu)
- Pasaka (Kufufuka kwake Yesu)
- Kupaa kwake Bwana (Yesu kuingia mbinguni)
- Pentekoste
- Watakatifu wote
[edit] Sikukuu za Uislamu
Sikukuu za kiislamu hufuata kalenda ya Kiislamu. Kwa hiyo tarehe za sikukuu hizi katika kalenda ya Gregori hubadilikabadilika.
- Ashurah tar. 1-10 muharram
- Idd-ul-Fitr mwisho wa ramadan
- Idd-ul-Adha tar. 10 dhu l-hija
- Mawlidi-ar-Rasul tar. 10 rabi' al-auwal
[edit] Sikukuu za Uhindu
- Diwali pia "Deepavali" - mwezi wa Oktoba au Novemba
[edit] Sikuu za Serikali
Hutofautiana kati ya nchi na nchi lakini mara nyingi huwa na:
- Mwaka Mpya
- 1 Mei
- sikukuu za kisiasa kama uhuru wa nchi, sikukuu ya kuzaliwa kwa mfalme au rais, kumbukumbukumbu ya mapinduzi n.k.