Taiwan
From Wikipedia
Taiwan (pia: Formosa) ni kisiwa cha Asia ya Mashariki katika Pasifiki. Iko upande wa kusini-mashariki ya China, kusini ya Japani na kaskazini ya Ufilipino. Jina la zamani la Taiwan ilikuwa "Formosa" (kireno: kisiwa kizuri, cha kupendeza)
Taiwan ni pia sehemu kubwa ya eneo la Jamhuri ya China iliyoko kisiwani Taiwan na pia kwenye visiwa vingine vidogo nje ya China bara.
Miji mikubwa ni Taipei na Kaohsiung.
Wakazi walio wengi ni Wachina wa Han. Kuna pia wakazi asilia.
Kisiwa kinadaiwa na Jamhuri ya Watu wa China kama eneo lake.
Makala hiyo kuhusu "Taiwan" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Taiwan kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |