Jamhuri ya China
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Misingi mitatu ya taifa (三民主義 San-min Chu-i) |
|||||
Wimbo wa taifa: Wimbo la taifa la Jamhuri ya China | |||||
Mji mkuu | Taipei (hali halisi)1 |
||||
Mji mkubwa nchini | Taipei | ||||
Lugha rasmi | Kichina (Guóyǔ) | ||||
Serikali
Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya China Waziri Mkuu |
Demokrasia Chen Shui-bian Annette Lu Su Tseng-chang |
||||
Tarehe za Kihistoria Jamhuri ilitangazwa Iliundwa Ilihamia Taiwan |
10 Oktoba 1911 1 Januari 1912 7 Desemba 1949 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
35,980 km² (137 ya) 10.3 |
||||
Idadi ya watu - 2006 kadirio - Msongamano wa watu |
23,036,087 (ya 472) 635/km² (ya 142) |
||||
Fedha | Dollar mpya ya Taiwan (NT$) (TWD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CST (UTC+8) not observed (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .tw | ||||
Kodi ya simu | +886 |
||||
1 Serikali ya Kuomintang ilitaja mji wa Nanking (China bara) kama mji mkuu rasmi 2 takwimu za 2006 |
Jamhuri ya China (pia: Taiwan) ni nchi ya visiwani katika Asia ya Mashariki upande wa kusini-mashariki ya China bara. Eneo lake ni kisiwa kikubwa cha Taiwan na visiwa vidogo mbele ya mwambao wa China bara.
[edit] Historia
Nchi jinsi ilivyo ni tokeo la vita ya wenyewe kwa wenyewe ya China iliyokwisha mwaka 1949 na ushindi wa Wakomunisti chini ya Mao Zedong na kuundwa kwa Jamhuri ya Watu wa China katika Beijing.
Wakomunisti walifukuza serikali ya chama cha Kuomintang iliyoongoza Jamhuri ya China. Jamhuri hii ilianzishwa mwaka 1912 na iliwahi kutawala China yote.
Mwaka 1949 serikali ya Kuomintang chini ya jenerali Chiang Kai-shek na mabaki ya jeshi lake ilihamia Taiwan walipoendelea kutawala. Wakomunisti walikosa nguvu ya kuwafuata hadi kwenye visiwa.
Hivyo serikali katika Taiwan iliendelea kujiita "serikali ya China" na kutangaza shabaha yake ilikuwa ukombozi wa China yote.
Hali halisi utawala wa Wakomunisti barani uliimarika na mipango yote kinyume chake ilionekana kama ndoto. Lakini kwa miaka minghi serikali ya Taipeh ilichukua nafasi ya China yote kimataifa
Jamhuri ya China ilikuwa kati ya nchi zilizoanzisha Umoja wa Mataifa mwaka 1945 na serikali ya Kuomintang iliendelea kushika kiti cha China hadi 1971. Tar. 25 Oktoba 1971 mkutano mkuu wa UM uliamua ya kuwa Jamhuri ya Watu wa China ni mwakilishi halisi wa China kwenye UM. Jamhuri ya China ilifukuzwa hivyo.
Siku hizi uhusiano kati ya China zote mbili ni vigumu. Wananchi wengi wa Jamhuri ya China wameanza kujitazama kama Wataiwan siyo Wachina tena. Nchi imefaulu sana kiuchumi. Lakini serikali ya Beijing inatazama Taiwan kama jimbo lililoasi.
[edit] Eneo
Sehemu kubwa ya eeno chini ya serikali ya Jamhuri ya China ni kisiwa cha Taiwan.
Upande wa magharibi kuna funguvisiwa tatu
- Visiwa vya Wavuwi ama Pescadores - (Penghu, 澎湖列島)
- Quemoy (Kinmen, 金門)
- Matsu (馬祖列島)
- Visiwa mbalimbali katika Bahari ya China visivyo na wakazi .
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Cyprus2 | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Oman | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China. |