Alexander Graham Bell
From Wikipedia
Alexander Graham Bell (3 Machi 1847 – 2 Agosti 1922) alikuwa mgunduzi wa mawasiliano ya simu. Alizaliwa katika mji wa Edinburgh nchini Uskoti lakini baadaye alihamia nchi za Kanada na Marekani. Baba yake alikuwa mwalimu wa watoto wenye matatizo ya kusikia na kuongea. Alifanikiwa katika jaribio lake la kwanza mwaka 1876.