Boris Leonidovich Pasternak
From Wikipedia
Boris Leonidovich Pasternak (10 Februari, 1890 – 30 Mei, 1960) alikuwa mwandishi na mshairi kutoka nchi ya Urusi. Ingawa aliandika mashairi kwa ujumla, anajulikana hasa kwa riwaya yake "Daktari Zhivago" iliyotolewa mwaka wa 1956. Mwaka wa 1958 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi lakini aliikataa kwa sababu ya upinzani katika nchi yake.