Dhaka
From Wikipedia
Dhaka ni mji mkuu wa Bangladesh pia mji mkubwa wa nchi mwenye wakazi 12,560,000 (mwaka 2005). Iko kando la mto Dhaleswari inayoendelea kuleta mafurko mara kwa mara wakati wa mvua za monsuni.
Miji ilipatikana katika eneo la Dhaka tangu karne ya 7 BK. Kabla ya kuja kwa Uislamu utamaduni wa eneo lilikuwa la Kihindu na Kibuddha. Wakati wa utawala wa Wamoghul idadi ya Waislamu iliongezeka. Dhaka ilikuwa na mchanganyiko wa dini hadi mgawanyo wa Uhindi wa 1947 wakati ambapo Wahindu walikimbia au kufukuzwa katika sehemu hii ya nchi si wengi tena waliobaki.
1947 Dhaka ilikuwa mji mkuu wa sehemu ya mashariki ya Pakistan. Baada ya uasi wa Pakistan ya Mashariki ikawa mji mkuu wa nchi mpya ya Bangladesh.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Dhaka" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Dhaka kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |