Frati
From Wikipedia
Mto Frati | |
---|---|
|
|
Chanzo | Uturuki ya Mashariki |
Mdomo | Ghuba ya Uajemi kwenye Shatt al Arab |
Nchi | Uturuki, Syria, Iraq |
Urefu | 2,800 km |
Kimo cha chanzo | 4,500 m |
Mkondo | 818 m³/s (wastani) |
Eneo la beseni | 765,831 km² |
Mto Frati (Kigiriki: Ευφράτης euphrátēs; Kiakkadi: Pu-rat-tu; Kiebrania: פְּרָת Pĕrāth; Kiaramu: ܦܪܬ Prâth; Kar.: الفرات al-furāt; Kituruki: Fırat; Kikurdi: فرهات, Firhat) ni mto mkubwa wa Asia ya magharibi. Pamoja na Hidekeli inatoka katika milima ya Uturuki ya Mashariki na kuunda eneo la Mesopotamia katika Iraq.
Katika Biblia imetajwa kama mto mmojawapo wa paradiso.
Frati ina urefu wa takriban 2,781 km. Baada ya kutoka katika nyanda za juu za Uturuki inaingia katika tambarare ya jangwa la Shamu na kuendelea katika Iraq inapopita kwenye maghofu ya Babeli. Karibu na mji wa Basra mto unaungana na mto Hidekeli na kuitwa Shatt al Arab hadi mdomo wake katika Ghuba ya Uajemi.
Mto Frati unapita katika maeneo makavu hivyo nchi zote unapopita zianjaribu kutumia maji yake kwa vituo vya kuvuta maji na malambo mbalimbali yaliyounda maziwa makubwa.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Frati" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Frati kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |