Kamerun (mlima)
From Wikipedia
Kamerun ni volkeno hai na mlima mkubwa nchini Kamerun mwenye kimo cha 4095 m juu ya UB. Majina mengine ni Fako (jina la kelele ya juu) au Mongo ma Ndemi ("Mlima Mkubwa").
Mlima uko karibi na Ghuba ya Guinea ya Atlantiki na mji wa bandari Douala.
Milipuko imeripotiwa katika miaka 1650, 1807, 1825, 1838, 1852, 1865, 1866, 1871, 1909, 1922, 1925, 1954, 1959, 1982 na 1999 BK. Kuna uwezekano ya kwamba tayari mbaharia Hanno wa Karthago alimaanisha mlima wa Kamerun alipoeleza habari za mlima wa "Gari la Miungu" uliotema moto kwa mwisho wa safari yake ya Afrika ya Magharibi mnamo mwaka 570 KK.