Kicheki
From Wikipedia
Kicheki ni lugha ya Kislavoni katika familia ya lugha za Kislavoni cha Magharibi inayotumiwa nchini Ucheki. Kuna wasemaji takriban milioni mbili nje ya Ucheki.
Kicheki ni lugha ya karibu na Kislovakia na Kisorbi. Kinaandikwa kwa alfabeti ya Kilatini.
Wageni hushtuka mara nyingi wakiona maneno bila vokali kwa mfano sentensi "Strč prst skrz krk". Sababu yake ni ya kwamba herufi za r na l zinaweza kuhesabiwa kama silabi (utaratibu unaofanana na "m" kama mwanzo wa neno mbele ya konsonanti katika lugha za Kibantu: m-fano, M-swahili) .
Sarufi inapanga nomino zote katika jinsia tatu.
Makala hiyo kuhusu "Kicheki" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kicheki kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |