Pablo Neruda
From Wikipedia
Pablo Neruda (12 Julai, 1904 – 23 Septemba, 1973) alikuwa mwanasiasa na mshairi kutoka nchi ya Chile. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Neftalí Ricardo Reyes Basoalto. Alikuwa balozi wa nchi yake katika nchi mbalimbali za Asia, Ulaya na Amerika ya Kusini. Mwaka wa 1971 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.