Chile
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: "Por la razón o la fuerza" (Kwa akili au nguvu) |
|||||
Wimbo wa taifa: Puro, Chile, es tu cielo azulado "Safi ee Chile ni anga lako ya buluu"' |
|||||
Mji mkuu | Santiago de Chile1 |
||||
Mji mkubwa nchini | Santiago de Chile | ||||
Lugha rasmi | Kihispania | ||||
Serikali
Rais
|
Jamhuri Michelle Bachelet |
||||
Uhuru Serikali ya kwanza ya uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa |
18 Septemba 1810 12 Februari 1818 25 Aprili 1844 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
756,950 km² (ya 38) 1.07%2 |
||||
Idadi ya watu - Juni 2006 kadirio - 2002 sensa - Msongamano wa watu |
16,432,674 (ya 60) 15,116,435 21/km² (ya 184) |
||||
Fedha | Peso (CLP ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
— (UTC-4) — (UTC-3) |
||||
Intaneti TLD | .cl | ||||
Kodi ya simu | +56 |
||||
1 The legislative body operates in Valparaíso 2 Includes Easter Island and Isla Sala y Gómez; does not include 1,250,000 km² of claimed territory in Antarctica |
Chile ni nchi ya Amerika Kusini. Eneo lake ni kanda ndefu nyembamba kati ya safu za milima ya Andes na Bahari ya Pasifiki. Imepakana na Peru, Bolivia na Argentina.
Sehemu za Chile ni pia maeneo ya Kisiwa cha Pasaka (Rapa Nui) na visiwa vya Kisiwa cha Salas y Gómez, Visiwa vya Juan Fernández (pamoja na kisiwa cha Robinson Crusoe), visiwa vya Desventuradas, Visiwa vya Ildefonso na vya Diego Ramirez. Chile inadai ya kuwa sehemu ya bara la Antaktika ni eneo lake.
[edit] Jiografia
Chile ina urefu wa 4,200 km kufuata pwani la Pasifiki na milima ya Andes. Umbali huu ni kama kutoka Cape Town kwenda Dar es Salaam. Lakini upana wa wastani wa eneo lake ni 180 km pekee. Sehemu nyembamba ya nchi ina upana wa 90 km, sehemu pana ina 240 km.
Nje ya maeneo penye uwanja mwembamba wa pwani nchi yote ni ya milima na mabonde. Sehemu kubwa ya nchi ina safu mbili za milima:
- Andes katika mashariki na
- Cordillera de la Costa (safu ya pwani) katika magharibi.
Katikati ya safu hizi mbili kuna bonde la kati (Valle Central) penye makazi ya idadi kubwa ya wananchi na ardhi yenye rutba ya kilimo.
Kuelekea kusini kimo cha nchi hushuka chini hadi kufikia chini ya uwiano wa bahari. Milima ya safu ya pwani huonekana sasa kama visiwa.
Katika kaskazini ya nchi hakuna bonde kubwa la kati. Nchi inapanda juu kutoka mwambao wa bahari hadi kuwa tambarare yenye kimo cha mita 1,000 - 1,500 m inayoendelea mpaka mwanzo wa safu ya Andes.
[edit] Milima
Andes za Chile ni kati ya milima ya juu duniani kuna vilele kadhaa juu ya 6,000m.
- Volkeno ya Nevado Ojos del Salado, 6,880 m (Región de Atacama)
- Cerro Tupungato, 6,800 m (Región Metropolitana)
- Volkeno ya Llullaillaco, 6,739 m (Región de Antofagasta)
- Volkeno ya Parinacota, 6,342 m (Región de Tarapacá)
- Volkeno ya Licancábur, 5,916 m (Región de Antofagasta)
- Descabezado Grande, 3,830 m (Región del Maule)
- Torres del Paine, 2,800 m (Región de Magallanes y de la Antártica Chilena)
- Volkeno ya Villarrica, 2,840 m (Región de la Araucanía)
- Volkeno ya Osorno, 2,652 m (Región de los Lagos)
- Volkeno ya Cerro Hudson, 1,905 m (Región de Aisén)
Makala hiyo kuhusu "Chile" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Chile kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |