Puerto Rico
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Kilatini: Joannes Est Nomen Eius; Kihispania: Juan es su nombre ("Jina lake ni Yohane ") |
|||||
Wimbo wa taifa: La Borinqueña | |||||
Mji mkuu | San Juan |
||||
Mji mkubwa nchini | San Juan | ||||
Lugha rasmi | Kihispania, Kiingereza | ||||
Serikali
Gavana
|
demokrasia Aníbal Acevedo Vilá |
||||
Uhuru established_dates = area = 9,104 |
{{{established_dates}}} | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
{{{area}}} km² (ya 169) 1.6 |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - 2005 sensa - Msongamano wa watu |
3,912,054 (ya 126) 3,913,054 434/km² (ya 21) |
||||
Fedha | Dollar ya Marekani (USD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
AST (UTC-4) No DST (UTC-4) |
||||
Intaneti TLD | .pr | ||||
Kodi ya simu | +1-787 and +1-939 |
Puerto Rico ni nchi katika Bahari ya Karibi ambayo ni eneo la kushirikishwa la Marekani katika visiwa vya Antili Kubwa. Iko upande wa mashariki ya Jamhuri ya Dominika na upande wa magharibi ya Visiwa vya Virgin. Jina la Puerto Rico humaanisha "bandari tajiri".
Ilikuwa koloni ya Hispania iliyovamiwa na Marekani tar. 25 Julai 1898 wakati wa Vita ya Marekani dhidi Hispania na kutawaliwa kama koloni hadi 1917 ambako watu wa Puerto Rico walipewa uraia wa Marekani na kiwango cha utawala wa mambo ya ndani. Tangu 1948 gavana imechaguliwa na watu si kuteuliwa tena na rais wa Marekani.
Funguvisiwa ya Puerto Rico inajumuisha kisiwa kikuu cha Puerto Rico pamoja na visiwa na funguvisiwa vidogo kama vile Mona, Vieques na Culebra.
Puerto Rico si jimbo kamili ya Marekani bali nchi inayojitawala katika mambo ya ndani ilhali siasa ya nje na mambo ya uchumi hutawaliwa na Marekani. Wakazi ni raia wa Marekani lakini hawashiriki katika uchaguzi wa rais. Kuna mwakilishi wa Puerto Rico katika bunge la Washington lakini hapigi kura.
Watu wa Puerto Rico humchagua Gavana na wabunge wao. Katika kura za 1967 na 1993 walikataa kutafuta uhuru lakini walikataa pia kuwa jimbo kamili la Marekani wakapendelea hali ya eneo la kushirikishwa.