Rasi ya Korea
From Wikipedia
Rasi ya Korea ni rasi kubwa katika Asia ya Mashariki. Inaingia takriban 1,100 km kutoka Asia bara ndani ya bahari ya Pasifiki. Bahari upande wa mashariki huitwa bahari ya Japani na upande wa magharibi huitwa Bahari Njano. Mlango wa bahari wa Korea hutenganisha Korea na Japani ukiunganisha bahari zote mbili za kando.
Tangu mwisho wa ukoloni wa Japani 1945 rasi iligawiwa kisiasa, kwanza kati ya kanda za kirusi na kimarekani. Tangu mwisho wa vita ya Korea tar. 27 Julai 1953 rasi imegawiwa kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.
[edit] Tazama pia
- Korea
- Korea Kaskazini (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea)
- Korea Kusini (Jamhuri ya Korea)