Korea Kaskazini
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Nchi tajiri na kubwa (강성대국) b | |||||
Wimbo wa taifa: Aegukka | |||||
![]() |
|||||
Mji mkuu | P'yŏngyang |
||||
Mji mkubwa nchini | Pyongyang | ||||
Lugha rasmi | Kikorea | ||||
Serikali | Udikteta Kim Il-sungc Kim Jong-ild Kim Yong-name Pak Pong-ju |
||||
Kuundwa kwa Ufalme wa Gojoseon Tangazo la uhuru bado chini ya Japani Ukombozi kutoka utawala wa Japani Jamhuri |
3 Oktoba 2333 KKa 1 Machi 1919 15 Agosti 1945 15 Agosti1948 9 Septemba 1948 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
120,540 km² (ya 98) 4.87 |
||||
Idadi ya watu - 2006 kadirio - [[As of |]] sensa - Msongamano wa watu |
23,113,019f (ya 48) n/a 190/km² (ya 55) |
||||
Fedha | Won ya Korea Kaskazini (₩) (KPW ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+9) (UTC) |
||||
Intaneti TLD | none (.kp reserved) | ||||
Kodi ya simu | +850 |
||||
c Alikufa 1994. d Kim Jong-il ni kiongozi wa kitaifa ingawa hana cheo kama mkuu wa nchi au mkuu wa serikali bali mwenyekiti wa kamati ya jeshi e Kim Yong-nam "Mkuu wa nchi kwa mambo ya nje". f chanzo: CIA World Factbook, Korea, North. Korea Kaskazini haitangazi takwimu g Legendary. h Symbolic. |
Korea ya Kaskazini (rasmi: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea) ni nchi ya Asia ya Mashariki iliyoko kwenye nusu ya kaskazini ya rasi ya Korea. Mji mkuu ni Pyongyang.
Imepakana na Korea Kusini, China na Urusi.
[edit] Historia
Korea Kaskazini kama nchi ya pekee ni tokeo la ugawaji wa Korea baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Korea iliyokuwa koloni ya Japan hadi 1945 iligawiwa na washindi Marekani na Urusi. Kila moja alianzisha serikali ya pekee kufuatana na itikadi yake katika kanda la utawala wake. Warusi waliacha serikali ya kikomunisti katika kaskazini na Waamerika waliacha serikali iliyochaguliwa katika kusini.
Katika vita ya Korea iliyofuata Korea ya Kaskazini iliweza kudumu kwa sababu ya msaada wa kijeshi wa China.
Kiongozi mkomunisti Kim Il-Sung alishika utawala akatawala kama dikteta kwa msaada wa chama cha kikomunisti na jeshi. Alipokufa mwaka 1994 mwanawake Kim Jong-Il aliandaliwa kuchukua nafasi yake.
Kim Il-Sung aliunda itikadi ya "Juche"; inaitwa falsafa ya kuendeleza Umarxisti lakini hali halisi ni itikadi inayotakiwa kutoa msingi kwa utawala wa dikteta. Ingawa ilidai kutafuta maendeleo ya kujitegemea Korea Kaskazini ilikuwa nchi iliyotegemea msaada kutoka Urusi kwa historia yake yote. Baada ya mwisho wa Umoja wa Kisovyeti msaada huu ulikwisha na Korea Kaskazini iliingia katika kipindi kigumu sana cha kiuchumi.
Leo hii nchi haiwezi kulisha watu wake hutegemea usaidizi wa vyakula kutoka jumuiya ya kimataifa.
Udikteta katika Korea Kaskazini ni ya kikomunisti kwa jina lakini una tabia za kidini ndani yake. Kim Il-Sung alitangazwa kuwa "rais wa milele"; Kim Jong-Il hatumii cheo rasmi isipokuwa "mwenyekiti wa kamati ya utetezi wa taifa" kinachomaanisha kitu kama "mkuu wa jeshi".
Katika mwaka 2006 Korea Kaskazini ililitekeleza mlipuko wa nyuklia.
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Cyprus2 | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Oman | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China. |