Toscana
From Wikipedia
Toscana ni moja kati ya majimbo 20 ya Italia. Iko katikati ya rasi ya Italia kaskazini ya Roma. Mji mkuu ni Firenze. Jumla ya wakazi ilikuwa 3,516,000 mwaka 2004. Eneo lake ni la 20,990 km².
Toscana huitwa jimbo zuri la Italia kwa sababu ya hali ya hewa, uzuri wa mabonde na milima na urithi wake wa kiutamaduni.
[edit] Jiografia
Toscana imepakana na majimbo ya Emilia-Romagna, Liguria, Tyrrhenia, Umbria, Marche na Latium. Sehemu kubwa ni eneo la vilima-vilima. Kunda tambarare katika bonde la mto Arno.
[edit] Wilaya
- Firenze ni mji mkuu au kwa Kiitalia "Capoluogo di regione"
- Arezzo
- Grosseto
- Livorno
- Lucca
- Massa-Carrara
- Pisa
- Pistoia
- Prato
- Siena