Utegili (fizikia)
From Wikipedia
Utegili katika lugha ya fisikia ni hali ya mada kama gesi ya kuionika.
Ikiwa gesi ni ya joto kali sana elektroni zake zinaanza kuachana na atomi zao. Tabia ya hali hii ni tofauti na hali ya gesi yenyewe. Elektroni zisizoshikwa na atomi pamoja atomi hizo katika hali ya ioni zote zinajibu kwa uga wa sumakuumeme.
Asilimia kubwa ya mada ulimwenguni iko katika hali ya utegili kwa sababu imo ndani ya nyota za angani.
Kwa ajili ya matumizi ya mitamboni hali ya utegili yaani ya kuionika husababishwa pia kwa leza au kwa uga wa sumakuumeme.