Visiwa vya Marshall
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: "Jepilpilin ke ejukaan" | |||||
Wimbo wa taifa: Forever Marshall Islands | |||||
![]() |
|||||
Mji mkuu | Majuro |
||||
Mji mkubwa nchini | Majuro | ||||
Lugha rasmi | Marshallese, Kiingereza | ||||
Serikali
Rais
|
Kessai Note |
||||
Uhuru kutoka Marekani |
21 Oktoba 1986 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
181 km² (ya 213) ‘‘(kidogo sana)’’ |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - 2003 sensa - Msongamano wa watu |
61,963 (ya 205) 56,429 326/km² (ya 28) |
||||
Fedha | US Dollar (USD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+12) (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .mh | ||||
Kodi ya simu | +692 |
Visiwa vya Marshall ni nchi ya visiwani ya Mikronesia katika Pasifiki ya magharibi. Nchi jirani katika bahari ni Nauru, Kiribati, Shirikisho la Mikronesia na eneo la Marekani la Kisiwa cha Wake. Atolli ya Majuro ina nafasi ya mji mkuu.
[edit] Jiografia
Eneo la visiwa vya Marshall ni safu mbili za visiwa au atolli zinazoelea sambamba:
- safu ya Ratak upande wa mashariki na
- safu ya Ralik upande wa magharibi.
Kwa jumla kuna visiwa na vipande vya atolli 1,150 katika eneo la bahari la 1,900,000 km².
[edit] Historia
Jina limetokana na nahodha Mwingereza John Marshall aliyetembelea eneo hili mwaka 1788 na kulichora katika ramani. Hata hivyo visiwa vilikaliwa tayari tangu karne nyingi na watu kutoka Mikronesia lakini jina la kizungu limebaki kwa ajili ya jumla ya visiwa. Mwisho wa karne ya 19 Ujerumani ulianzisha ukoloni juu ya visiwa ukaviunganisha kiutawala na Guinea Mpya yya Kijerumani. Katika vita kuu ya kwanza ya dunia vilitwaliwa na Japani iliyoendelea kutawala visiwa kama eneo lindwa kwa niaba ya shirikisho la mataifa. Baada ya vita kuu ya pili ya dunia vilikuwa eneo chini ya Marekani.
1979 visiwa vimepata madaraka ya kujitawala na kupokea uhuru kufuatana na azimio la Umoja wa Mataifa 1990.
[edit] Majaribio ya kinyuklia
Kuanzia 1946 Marekani ilitumia visiwa kwa ajili ya majaribio ya mabomu ya nyuklia. Hadi 1958 ilitokea milipuko 6,913 kwenye atolli za Bikini na Eniwetok. Hadi leo kuna wakazi wa visiwa wanavyoteswa na maradhi yaliyosababishwa na mnurulisho wa mabomu haya. Bikini haitawezekana kukaliwa na watu kabla ya mwaka 2050, Eniwetok haifai kwa makazi ya kibinadamu kwa miaka 24,000 inayokuja.