Yordani (mto)
From Wikipedia
Mto wa Yordani | |
---|---|
|
|
Chanzo | Mlima Hermoni (mpakani wa Israel na Lebanon]]) |
Mdomo | Bahari ya Chumvi 400 m chini ya uwiano wa bahari |
Nchi | Lebanon, Syria, Israel, Yordania, Palestina |
Urefu | 400 km (170 km mwendo wa ndege) |
Kimo cha chanzo | takriban 300 m juu ya UB |
Eneo la beseni | km² |
Yordani (Kiebrania: נהר הירדן nehar hayarden, Kiarabu: نهر الأردن nahr al-urdun) ni mto mdogo katika Mashariki ya Kati lakini ni kati ya mito inayojulikana sana duniani kwa sababu imetajwa mara nyingi katika Biblia. Kwa sehemu kubwa ya njia yake ni mpaka kati ya ufalme wa Yordani upande wa mashariki na maeneo ya Palestina na Israel upande wa magharibi. Katika dini za Uyahudi na Ukristo Yordani ina maana ya kidini.
Chanzo cha Yordani ni mito minne inayoanza karibu na mlima Hermoni mpakani wa Israel, Lebanon na Syria. Mito ya chanzo inaungana katika Israel ya kaskazini. Yordani hupita Galilea na kutelemka kwa kunyoka mara nyingi hadi Bahari ya Chumvi. Mdomo wake uko 400 m chini ya usawa wa bahari hivyo Yordani ni mto wa duni kabisa duniani.
Kiasi cha maji kwenye sehemu ya kusini ya mto kimepungua sana kwa sababu Israel inavuta sehemu kubwa ya maji na kuitumia kwa ajili ya matumizi kibinadamu katika miji yake.