Yordani
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: {{{national_motto}}} | |||||
Wimbo wa taifa: عاش المليك ' ash al-malik "Heri kwa mfalme" |
|||||
Mji mkuu | Amman |
||||
Mji mkubwa nchini | Amman | ||||
Lugha rasmi | Kiarabu | ||||
Serikali | Ufalme wa Kikatiba Abdullah II Marouf al-Bakhit |
||||
Uhuru Tarehe |
25 Mei 1946 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
92,342 km² (ya 112) -- |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - 2003 sensa - Msongamano wa watu |
5,350,000 (ya 106) 4,755,000 64/km² (ya 131) |
||||
Fedha | Dinar ya Yordani (JOD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
UTC+2 (UTC+2) UTC+3 (UTC+3) |
||||
Intaneti TLD | .jo | ||||
Kodi ya simu | +962 |
Yordani (pia: Jordan, Jordani Kiar.; الأردنّ }} "al-urdun") ni ufalme wa Kiarabu katika Mashariki ya Kati. Jina rasmi ni Ufalme wa Kihashemi wa Yordani (Kiar.: المملكة الأردنية الهاشمية ) kutokana na familia ya kifalme. Imepakana na Syria, Iraq, Saudi Arabia na Israel. Ina pwani fupi kwenye Ghuba ya Aqaba ya Bahari ya Shamu.
Mji Mkuu ni Amman. Jina la nchi limetokana na mto Yordani ambao ni mpaka wake upande wa magharibi na Israel na eneo la Palestina ya leo.
Sehemu kubwa ya nchi ni jangwa.
[edit] Historia
Nchi ilianzishwa kwa jina la "Transjordan" (ng'ambo ya mto Yordani) kama sehemu ya eneo la Palestina lililotawaliwa na Uingereza kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa baada ya 1918. Waingereza waliamua kutanganisha eneo na Palestina upande wa magharibi ya mto Yordani na kuiweka tangu 1921 chini ya mamlaka ya Abdullah bin al-Husayn wa familia ya Wahashemi aliyekuwa mtoto wa Sharif wa Makka wa mwisho kabla ya kutwaliwa kwa mji huu na Wasaudi. Kwa hatua hii Uingereza ililenga kuimarisha uhusiano wake na makabila ya Waarabu wa jangwa. Abdullahi alitawala awali kwa cheo cha emir baadaye kama mfalme wa "Transjordan".
Jeshi lake lilishiriki katika vita ya mgawanyo wa Palestina na Israel 1948/1949 na kushika sehemu ya Palestina isiyotawaliwa na Israel. Baada ya vita ya siku sita ya 1967 maeneo yote upande wa magharibi ya mto Yordani yalipotelewa na mfalme Hussein mfuasi wa Abdallah tangu 1952 mwishowe aliacha madai yote ya utawala juu ya sehemu hizi.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Yordani" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Yordani kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |