Ganga (mto)
From Wikipedia
Mto Ganga (Ganges) | |
---|---|
|
|
Chanzo | barafuto ya Gangotri |
Mdomo | Ghuba ya Bengali |
Nchi za beseni ya mto | India, Bangladesh |
Urefu | 2,510 km |
Kimo cha chanzo | 7,756 m |
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | 14,270 m³/s |
Eneo la beseni (km²) | 907,000 km² |
Ganga (Kisanskrit गङ्गा, gaṅga) ni mto mkubwa katika Uhindi wa Kaskazini. Mto una uefu wa 2,511 km unapita nchi za Uhindi na Bangla Desh (Asien).
Chanzo chake ni katika milima ya Himalaya inapokutana mito ya Alaknanda na Bhagirathi. Kutoka hapa inaendelea kuelekea kusini-mashariki hadi tambarare ya Bengali. Nchini Bangla Desh inaunganika na mto Brahmaputra na kuwa na delta kubwa hadi kuingia katika Bahari Hindi.
[edit] Ganga na dini
Katika imani ya Uhindu Ganga ni mto mtakatifu. Huabudiwa pia kama mungu wa kike. Wafuasi wa dini ya Uhindu mara nyingi wanajaribu kuhiji mtoni kabla ya kufa wakitumaini ya kwmaba maiti itachomwa na majivu kumwagika mtoni. Kuoga mtoni kunatazamiwa kama bafu ya kuondoa dhambi.