Genghis Khan
From Wikipedia

Genghis Khan (tamka: Chingis Khan, * takriban 1162 – + 18 Agosti, 1227) alizaliwa kama Temujin akawa mfalme mkuu wa Mongolia maarufu katika dunia nzima.
Kwao wengi, Genghis Khan ni sawa na ushindi katili na ya kinyama. Wamongolia siku hizi wanamwona kama Baba yao wa Taifa. Alitumia miaka mingi kuunganisha na kueneza makabila mengi ambayo yalikuwa wakazi wa eneo ambalo sasa linaitwa Mongolia. Baadhi ya wanahistoria wanasema kwamba alikuwa na kichwa kizuri cha kijeshi kuliko karibu watu wote wengine katika historia ya dunia. Alianzisha ufalme wa Mongolia ambao wengi wanasema ulikuwa eneo kubwa lililounganishwa ambalo halijawahi kupitwa duniani, kutoka mwaka 1206 mpaka kifo chake mwanzoni mwa kipindi cha baridi 1227.