Isaac Newton
From Wikipedia
Isaac Newton (4 Januari, 1642 – 31 Machi, 1727) alikuwa mwanahisabati na mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Anakumbukwa kama mwanasayansi maarufu duniani kutokana na michango yake mbalimbali katika sayansi. Ndiye aliyegundua tawi la calculus na nadharia ya mwendo. Newton alipata shahada yake ya kwanza mwaka 1665 na ile ya uzamili mwaka 1668. Mchango mwingine wa Isaac Newton upo katika nadharia ya mwanga, kuona na jinsi rangi zinavyotokea. Nadharia zake zote aliziweka katika vitendo na kukubalika na ndizo zitumikazo hadi leo.