Lagos
From Wikipedia
Lagos ni mji mkubwa wa Nigeria. Ilikuwa mji mkuu wa nchi hadi 1991. Ikiwa na wakazi takriban milioni 9 katika eno la jiji na milioni 12 - 15 katika rundiko la mji ni kati ya miji mikubwa zaidi ya Afrika; inaweza kuwa na nafasi ya pili baada ya Kairo (Misri).
[edit] Jiografia
Lagos iko mwambaoni wa Ghuba ya Guinea; eneo la jiji ni pamoja na wangwa wa Lagos, funguvisiwa ndani ya maji ya wangwa na sehemu za bara. Visiwa vikubwa ni Lagos Island, Ikoyi, and Victoria.
[edit] Historia
Lagos ilianzishwa kama kijiji cha Wayoruba ikaendelea kukua kutokana na na biashara, bandari yake na kipindi kama mji mkuu wa Nigeria. Nafasi ya mji mkuu ilichukuliwa na Abuja lakini hadi leo Lagos inaendelea kuwa mji mkuu wa biashara na uchumi nchini.
Inaaminiwa ya kwamba Kisiwa cha Lagos kilikaliwa na wavuwi na wakulima Wayoruba tangu karne ya 14. Katika karne ya 15 eneo lilikuwa kwa muda chini ya ufalme wa Benin. Wakati ule lilitwa "Eko".
Mwaka 1472 mbaharia Mreno Ruy de Sequeira alifika Eko akaanzisha kituo cha biashara lililoitwa "Lagos" - kwa Kireno neno hili lamaanisha "maziwa" ni pia jina la mji Lagos katika Ureno ya kusini. Katika karne zilizofuata Lagos pamoja na utajiri wa Oba ilikua kutokana na bishara ya watumwa.
Katika karne ya 19 Waingereza walijaribu kukandamiza biashara hii ya watumwa katika Afrika ya Mashariki . 1841 Oba mpya aliyeitwa Akitoye alipiga biashara ya watumwa marufuku lakini alipinduliwa kwa sababu ya upinzani wa wafanyabiashara wenyeji. Akitoye aliomba usaidizi wa Uingereza. Manowari za kiingereza walishambulia Lagos tar. 26 na 27 Desemba 1852 na kumrudisha mfalme. Matatizo ya biashara ya watumwa yaliendelea na Waingereza walichukua kisiwa cha Lagos na kuifanya kwanza eneo lindwa halafu koloni. Oba alibaki na madaraka machache.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Lagos" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Lagos kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |