Mexico (mji)
From Wikipedia
Jiji la Meksiko (Kihisp.: Ciudad de México) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa nchi ya Mexiko. Iko kwenye nyanda za juu ya Mexiko kwenye kimo cha 2000 m juu ya UB katika bonde ndefu linalopakana na milima mirefu. Kati ya milima hii ni volkeno za Popocatepetl und Iztaccihuatl na nyororo ya Sierra Nevada.
Mji wa Mexiko ni pia mkoa wa kujitegema huitwa mara nyingi na Wamexiko wenyewe "Mexico DF" au kwa kifupi "DF" (DF = Distrito Federal, Mkoa wa Shirikisho).
Idadi ya wakazi ni milioni 8.7 na pamoja na mitaa ya karibu idadi inafikia karibu milioni 22. Ni kati ya miji mikubwa kabisa duniani.
[edit] Historia
[edit] Tenochtitlan
Historia ya mji ulianza mwaka 1325. Wakati ule kikosi cha Azteki wahamiaji walifika kwenye ziwa la Texcoco na kujenga makao kwenye kisiwa ziwani wakaita mji "Tenochtitlan".
Kuna hadithi ya kale juu ya kuundwa kwa Tenochtitlan ambayo ni mji wa Kiazteki uliotangulia Mexiko City.
Zamani ile Waazteki waliishi maisha ya kuhamahama na kutafuta mahali pa kujenga mji wa kudumu. Mungu wao Huitzilopochtli aliwaambia wamtafute anayekalia mpungate (kakati) na kushika nyoka. Mpungate utapatikana kwenye mwamba katika kisiwa ziwani. Hadithi yaendelea kusema ya kwamba baada ya matembezi ya miaka 200 walikuta ziwa la Texcoco penye mwamba na mpungate. Walipokaribia tai aliyeshika nyoka akaketi kenye mpungate huu.
Baada ya kupokea ishara hiyo waliunda mji wao wa Tenochtitlan uliokuwa baadaye mji mkuu wa Dola la Azteki. Ulikuwa na wakazi 300,000 wakati wa kufika kwa Wahispania mwaka 1519.
Mw. 1519 alifika Mhispania Hernan Cortez pamoja na jeshi ya askari 450. Baada ya kupokelewa vizuri na mfalme wa Azteki Montezuma walimkamata kama mfungwa na kuchukua dhahabu kutoka mahekalu. Wenyeji wa mji waliwashambulia na kuua Wahispania wengi. Cortes aliweza kukimbia akarudi na jeshi mpya akaweza kuteka mji tar. 13 Agosti 1521 na kuuharibu kabisa.
[edit] Mji wa Mexiko
Wahispania walianzisha mji mpya juu ya maghofu ya mji wa kale. Makanisa yalijengwa mahali pa mahekalu ya kale. Tangu 1525 mji wa Mexiko ulikuwa mahali pa serikali ya nchi, tangu 1535 mji mkuu wa "Ufalme Mdogo wa Hispania Mpya". Koloni za Hispania za Guatemala, Kuba, Florida na hata Ufilipino katika Asia yalitawaliwa kutoka hapa.
Mji ulikuwa mji mkuuwa nchi huru tangu 1821. Katika karne ya 20 ilikua haraka sana.