Mkoa wa Kagera
From Wikipedia
Mkoa wa Kagera ni mkoa wa kaskazini-magharibi kabisa katika Tanzania. Jina lake linatokana na mto Kagera.
Mkoa wa Kagera umepakana na Burundi, Rwanda na Uganda upande wa Magharibi na Kaskazini. Upande wa Kusini umepakana na mikoa mengine ya Tanzania ya Kigoma, Shinyanga na Mwanza. Eneo lake ni 28,953 km² za nchi kavu na 11,885 km² za maji hasa ya Viktoria Nyanza, jumla 40,838 km².
Mkoa wa Kagera uko mnamo 1000 m juu ya uwiano wa bahari.
Makao makuu ya mkoa ni mji wa Bukoba.
Kuna wilaya sita za Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini, Muleba, Karagwe, Ngara na Biharamulo.
Sensa ya mw. 2003 imeonyesha idadi ya wakazi kuwa 2,003,888 inayoendelea kuongezeka asilimia 3.1% kwa mwaka.
[edit] External links
- (en) Kagera – Bukoba – the official webguide
- (en) – Tourist Office Bukoba / Kagera
- (en) United Republic of Tanzania: Kagera Region
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |