Rhine
From Wikipedia
Rhine (Rhein) | |
---|---|
|
|
Chanzo | Grisons (Uswisi) |
Mdomo | Bahari ya Kaskazini katika Uholanzi |
Nchi | Uswisi, Lichtenstein, Austria, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi |
Urefu | 1,320 km |
Kimo cha chanzo | 2,344 m |
Mkondo | 2230 m³/s |
Eneo la beseni | 185,000 km² |
Rhine (tamka: rain) (kwa Kijerumani "Rhein", Kifaransa "Rhin" na Kiholanzi "Rijn") ni kati ya mito mirefu ya Ulaya.
[edit] Chanzo na nchi inapopita
Ina chanzo chake katika milima ya Uswisi. Inapita katika Uswisi, Ujerumani na Uholanzi; mwendo wake ni pia mpaka kati ya Uswisi na Liechtenstein, Uswisi na Austria halafu Ujerumani na Ufaransa.
Mpakani kati ya Uswisi na Ujerumani mto inapita katika ziwa la Konstanz (au: Bodensee).
[edit] Njia ya maji
Kuanzia mji wa Rheinfelden hadi Rotterdam kwa urefu wa zaidi ya 800 km mto unapitika kwa meli za mtoni.
Usafiri mtoni ni muhimu kwa ajili ya viwanda vingi vilivyopo kando la mto.
Kihistoria Rhine pamoja na mto Danubi ilikuwa mpaka wa kakazini ya Dola la Roma.
[edit] Delta ya Rhine
Ndani ya Uholanzi mto hujigawa kuwa na mikono mikubwa miwili inayoitwa Waal na Lek. Mbele ya mji wa Rotterdam inaungana tena kuwa mto mmoja.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Rhine" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Rhine kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |