Uholanzi
From Wikipedia
|
|||||
Hadabu ya Taifa: Je maintiendrai (Kifaransa) Kiswahili, Nitastahimili |
|||||
Lugha za Taifa |
Kiholanzi kwa mkoa wa Friesland: Kifrisi |
||||
Mji Mkuu | Amsterdam | ||||
Makao wa Serikali | Den Haag | ||||
Malkia | Beatrix van Oranje Nassau | ||||
Waziri Mkuu | Jan Peter Balkenende | ||||
Eneo - Jumla - % Maji |
41,526 km² 18.41 |
||||
Umma - Jumla - msongamano]] |
16,407,476 (Julai 2005) 395/km² |
||||
GDP - Jumla - kwa kipimo cha umma |
$625 bilioni $ 30,500 |
||||
Uhuru - Tangazwa - Kiriwa |
Kutoka Hispania Julai 26, 1581 Januari 30, 1648 |
||||
Fedha | Euro € EUR | ||||
Saa za Eneo | UTC +1 | ||||
Wimbo wa Taifa | Wilhelmus | ||||
TLD mtandao | .nl | ||||
Kodi ya simu | 31 |
Uholanzi ni nchi katika Ulaya wa Magharibi. Imepakana na Ujerumani upande wa mashariki, Ubelgiji upande wa kusini na Bahari ya Kaskazini (North Sea) upande wa magharibi na kaskazini. Uholanzi ni sehemu ya "Ufalme wa Nchi za Chini" (Kingdom of the Netherlands) pamoja na kisima cha Aruba na Visima vya Karibi vya Uholanzi.
Jina la Uholanzi limetokana na “Holland”, eneo la magharibi la nchi hii. Watu wengi hutumia jina hili, lakini wakazi wenyewe wanaiita nchi yao “Nederland” inayomaanisha "nchi ya chini". Kwa kweli, sehemu kubwa ya Uholanzi ni chini ya bahari. Waholanzi wamejenga maboma kuzuia maji yasienee yakifurika.
Contents |
[edit] Jiografia
Akifika Uholanzi kwa uwanja wa ndege wa Schiphol, msafiri atastaajabu na nchi ya tambarare. Kwa kweli, kuna sehemu zenye vilima, lakini sehemu kubwa zaidi ya Uholanzi ni tambarare. Mahali pa juu kabisa nchini ni Kilima cha Vaals, upande wa kusini wa mkoa wa Limburg, kwa 322 m. Mahali pa chini kabisa ni karibu na Niewerkerk aan de IJssel, mkoa wa Zuid Holland, kwa -6.76 m (mita 6.76 chini ya usawa wa wastani wa bahari).
Vipande vikubwa vya nchi vimepatwa kwa maji. Kufanya hii boma linajengwa linalozunguka ziwa au sehemu ya bahari kisha maji yanavutwa kwa bomba. Mahali kati ya boma huitwa “polder”. Mkoa mmoja wote, Flevoland, umepatwa kwa maji ya “Zuiderzee” (Bahari ya Kusini). Kwa sababu ya hii watu husema: “Mungu aliumba dunia lakini Waholanzi waliumba Uholanzi.” Hata sasa sehemu muhimu ya Uholanzi ni maji: 18%.
Maboma mengine makubwa yamejengwa upande wa kusini magharibi wa nchi ili ya kuzuia maji yasienee mikoa ya Zeeland na Zuid Holland. Mradi huu huitwa “Deltawerken” au Ujenzi wa Delta. “Oosterscheldekering” au boma la mto wa Oosterschelde ni jengo linaloshangaza. Urefu wake ni 9 km na katikati yake kuna malango makubwa 62 ambayo hujifunga wenyewe kila wakati ambapo maji ya bahari yakifura zaidi ya 3 m. Barabara kuu inapitia juu ya boma hili.
[edit] Mikoa
Uholanzi umegawanyika na mikoa 12. Kila mkoa unatawaliwa na gavana ambaye huitwa “Commissaris van de Koningin” isipokuwa yule wa Limburg ambaye huitwa “Gouverneur”. Mikoa na miji mikuu yao ni :
Mkoa | Mji mkuu |
---|---|
Groningen | Groningen |
Friesland | Leeuwarden |
Drenthe | Assen |
Overijssel | Zwolle |
Gelderland | Arnhem |
Utrecht | Utrecht |
Flevoland | Lelystad |
Noord-Holland | Haarlem |
Zuid-Holland | Den Haag (The Hague) |
Zeeland | Middelburg |
Noord-Brabant | ’s-Hertogenbosch (Den Bosch) |
Limburg | Maastricht |
[edit] Miji mikubwa
Mji | Wakazi |
---|---|
Amsterdam | 742,011 |
Rotterdam | 600,000 |
Den Haag | 476,000 |
Utrecht | 281,569 |
Eindhoven | 209,399 |
[edit] Mito
Mito mikubwa kadhaa inaingia Uholanzi na kutiririka katika Bahari ya Kaskazini. Mto Rijn (Rhine) unaingia kwa Tolkamer upande wa mashiriki, na karibu na Nijmegen Mto Waal unajitenga ambao unachukua 70% ya maji. Mto IJssel unajitenga karibu na Westervoort na kwenda upande wa kaskazini. Mto Maas (Meuse) unaingia Uholanzi upande wa kusini wa Limburg, na karibu na Mook unageuka upande wa magharibi. Mto Schelde unaingia upande wa kusini wa Zeeland.
[edit] Viungo vya nje
[edit] Historia, jiografia na siasa
- Overheid.nl - Lango rasmi la serikali ya Uholanzi
- Ramani na takwimu
- Mikoa ya Uholanzi
- CBS - Takwimu rasmi
- Makala ya Encarta kuhusu Uholanzi
- Government.nl - Tovuti rasmi ya serikali ya Uholanzi
- CIA - The World Factbook -- Netherlands
- Habari za Uholanzi: Radio Netherlands - Redio ya Uholanzi kwa lugha ya Kiingereza
[edit] Kusafiri
- Kiongozi cha Wikitravel cha kusafiria Uholanzi
- World66's guide to the Netherlands - Kiongozi cha kusafiri kinachoandikwa na watumiaji.
- Kiongozi cha kusafiri katika Uholanzi
- Picha za Uholanzi
- Just Landed Netherlands - Habari za manufaa kwa kuhamia Uholanzi
[edit] Viungo anuwai
- Ujenzi wa Delta kwa mtandao
- Keukenhof Bustani za Maua - Picha nzuri mno za bustani za maua katika Uholanzi.
- Familia ya kifalme ya Uholanzi
- Kiholanzi kwa wasemao Kiingereza
- Orodha ya majengo marefu 1500 katika Uholanzi
Nchi za Umoja wa Ulaya | ||||
---|---|---|---|---|
Austria | Cyprus | Denmark | Estonia | Finland | Hungaria | Ireland | Italia | Latvia | Lithuania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Hispania | Sweden | Ubelgiji | Uceki | Ufaransa | Ugiriki | Uholanzi | Uingereza| Ujerumani | Ureno Nchi zinazoandaa uanachama: Bulgaria | Romania
|