Ayatollah
From Wikipedia
Ayatollah (kiajemi: آيت الله, kiar.: آية الله ayatu 'llah - "alama ya Allah/Mungu") ni cheo cha kiongozi wa kidini katika Uislamu wa Shia hasa nchini Uajemi na pia Iraq.
Cheo cha ayatollah hakilingani na kuhani au askofu katika dini nyingine. Kinafanana zaidi ya profesa wa chuo kwa sababu ayatollah hutambuliwa baada ya kumaliza masomo yake na kufundisha kwa muda fulani. Akionekana anajua mambo yake anaheshimiwa na akina ayatollah waliomtangulia ataanza kuitwa hivyo.
Wachache huitwa "ayatollah mkubwa" wakikubaliwa na wafuasi wengi sana pia na wenzao.
Ayatollah aliyejulikana sana duniani alikuwa Ruhollah Khomeini (17 Mei 1900 - 3 Juni 1989) aliyeanzisha mapinduzi ya kiislamu nchini Uajemi na kuwa kiongozi wa jamhuri ya kiislamu.
Mwingine ni Ayatollah Mkubwa Ali Al-Hoessein al-Sistani ambaye ni kiongozi mkuu wa Washia nchini Iraq.