Martinique
From Wikipedia
Martinique ni kisiwa cha Antili Ndogo katika Bahari ya Karibi. Ni eneo la ng'ambo la Ufaransa na mkoa (departement)wa Ufaransa. Eneo lake ni 1,128 km². Idadi ya wakazi ni takriban lakhi 4. Takriban nusu wao ni wa asili ya Kiafrika ikiwa wazee wao walipelekwa hapa kama watumwa kwa ajili ya kazi za mashamba ya miwa. Kikundi kikubwa cha pili ni watoto wa Wahindi waliopelekwa Martinique kwa kazi ya mashamba baada ya mwisho wa utumwa.
Mji mkuu ni Fort-de-France. Miji mingine ni pamoja na Sainte-Anne na St. Pierre (iliyoharibiwa na mlipuko wa volkeno ya Mont Pelee mwaka 1902).
Martinique ni maarufu kwa muziki yake ya zouk. Mwanamuziki mashuhuri wa muziki hii ni Kassav.
[edit] Tazama pia
- Guadeloupe ni eneo nyingine ya Ufaransa katika Bahari ya Karibi.