Mashariki ya Kati
From Wikipedia

Mashariki ya Kati ni namna ya kutaja sehemu kubwa ya Asia ya Magharibi.
Kwa kawaida nchi zifuatazo huhesabiwa humo:
- Nchi za Bara Arabu pamoja na Saudia,Kuwait, Falme za Kiarabu, Yemen na Oman
- Nchi za Shamu ya kihistoria pamoja na Syria, Lebanon, Israel na Palestina, Yordani
- Iraq
- Uajemi
- Uturuki
- Misri (ambayo ni upande wa Afrika isipokuwa rasi ya Sinai)
Nchi hizi zinatajwa pamoja kwa sababu zina historia ya pamoja na utamaduni ni wa karibu kati yao.
[edit] Matatizo ya jina hili
Jina la "Mashariki ya Kati" limesambazwa kutokana na kawaida ya Kiingereza na kutafsiriwa katika lugha mbalimbali. Lina matatizo kadhaa yanayotakiwa kujulikana hata tukiendelea kutumia jina:
- kuna namna mbalimbali za kutaja nchi za zaida zinazohesabiwa humo au la (kwa mfano: wengine huhesabu pia nchi za Asia ya Kati kama vile Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan n.k.)
- jina ni tamko la Kiulaya: nchi hizi ziko upande wa mashariki kwa mtu aliyeko Ulaya. Kutoka Uswahilini ingekuwa zaidi "Kaskazini ya Kati"
- matumizi ya jina yamebadilika: zamani Kiingereza kilitofautisha kati ya
- "Mashariki ya Karibu",
- "Mashariki ya Kati" na
- "Mashariki ya Mbali"
kikimaanisha
-
- a) nchi za Bara Arabu na jirani;
- b) nchi za Uhindi na jirani
- c) nchi za Asia ya Mashariki.
Lugha mbalimbali za Ulaya Bara kama Kijerumani zinaendelea kutumia majina haya matatu vile. Pia wataalamu wa historia kwa Kiingereza hupendelea kutofautisha kati ya "Mashariki ya Karibu" na "Mashariki ya Kati".
Categories: Mbegu | Jiografia | Asia