Kitajiki
From Wikipedia
Kitajiki (тоҷикӣ / تاجیکی / tamka "tojiki" au забони тоҷикӣ / زبان تاجکی / tamka "zabone tojiki") ni lugha rasmi nchini Tajikistan katika Asia ya Kati. Kitajiki ni inatajwa mara nyingi kama lahaja ya Kiajemi. Wasemaji wa Kitajiki wanaelewana bila matatizo na wasemaji wa Kiajemi nchini Uajemi au wasemaji wa Kidari nchini Afghanistan.
Lugha huandikwa katika Tajikistan kwa herufi za Kikyrili kama Kirusi. Hadi miaka ya 1920 iliandikwa kwa herufi za Kiarabu.
Kuna pia wasemaji wa Kitajiki katika Urusi na katika Uzbekistan.
Kama Kiajemi ni sehemu ya lugha za Kiirani kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya.