Kirusi
From Wikipedia
Kirusi (русский язык russkii yazik) ni moja kati ya lugha za Kislavoni cha Mashariki yenye wasemaji wengi kati ya lugha zote za Kislavoni.
Kirusi ni lugha rasmi katika Urusi na pia lugha rasmi katika nchi jirani za Belarus, Kazakhstan na Kirgizia. Wasemaji wa Kirusi wako katika nchi zote zilizokuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi 1991. Kuna pia Warusi katika nchi za magharibi kwa sababu wakati wa ukomunisti palikuwa na wakimbizi waliotoka nje ya Urusi kwa sababu za kisiasa.
Watu wengi duniani wamejifunza Kirusi kwa sababu ilikuwa lugha ya kimataifa kati ya nchi zilizoshikamana na Umoja wa Kisovyeti. Wanafunzi wengi kutoka nchi mbalimbali za Afrika walipata elimu ya juu kwenye vyuo vikuu vya Umoja wa Kisovyeti kwa lugha ya Kirusi.
[edit] Viungo vya Nje
Makala hiyo kuhusu "Kirusi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kirusi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |