Uzbekistan
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: Wimbo la Taifa | |||||
Mji mkuu | Tashkent |
||||
Mji mkubwa nchini | Tashkent | ||||
Lugha rasmi | Kiuzbeki | ||||
Serikali | Jamhuri Islom Karimov Shavkat Mirziyoyev |
||||
Uhuru Ilitangazwa Formation Recognized Completed |
1747 kama Dola la Bukhara, Dola la Kokand, Khwarezm 1 Septemba 1991 8 Desemba 1991 25 Desemba 1991 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
447,400 km² (ya 56) 4.9 |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
26,593,000 (ya 44) 59/km² (ya 136) |
||||
Fedha | Som ya Uzbekistan (UZS ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
UZT (UTC+5) not observed (UTC+5) |
||||
Intaneti TLD | .uz | ||||
Kodi ya simu | +998 |
Uzbekistan ni nchi ya Asia ya Kati. Mji mkuu na pia mji mkubwa ni Tashkent.
Imepakana na Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Turkmenistan. Kuna takriban wakazi 26,600,000.
Watu walio wengi (zaidi ya 70 %) hutumia lugha ya Kiuzbeki ambacho ni kati ya lugha za Kiturki. Kuna vikundi vingi vidogo zaidi vya utamaduni tofauti kama vile Warusi (5,5 %), Watajiki (5,1 %), Wakazakhi (4,2 %), Watartari (2 %), Wakarakalpaki (2 %), Wakorea (1,1 %) na mengine.
Hadi mwaka 1991 Uzbekistan ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet. Ilijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiuzbeki" hadi 1991.
[edit] Historia
Uzbekistan ni nchi ya historia ndefu. Ferghana, Tashkent, Bukhara, Khwarezm na Samarkand zilikuwa vitovu vya utamaduni wa kibinadamu tangu milenia ya pili KK. Katika karne kabla na baada ya Kristo eneo lilijulikana kama Sogdiana na Baktria. Miji yake ilikuwa na utajiri kutokana na biashara ya misafara kwenye barabara ya hariri kati ya China na Mashariki ya Kati.
Baadaye ilitawaliwa na milki mbalimbali za nje kama Uajemi. Kuanzia uenezi wa Uislamu watu ba Uzbekistan waligeukia dini hii mpya. Katika karne ya 14 jemadari Timur alijenga milki kubwa na kuharibu nchi za magharibi hadi Uturuki. Alipamba mji mkuu wake Samarkand kwa majengo mazuri.
Baada ya Timur milki yake iliporomoka na Uzbekistan ilitawaliwa na madola mbalimbali ya kieneo yaliyokuwa hasa eneo la mji muhimu.
Katika karne ya 19 Urusi ulieneza athira yake kuelekea kusini na kuunganisha madola ya Uzbekistan na milki yake.
Baada ya mapinduzi ya Urusi ya 1917 Uzbekistan ikawa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi kuporomoka kwake 1991.
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Cyprus2 | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Oman | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China. |