Mao Zedong
From Wikipedia
Mao Zedong (* 26 Desemba 1893 / + 9 Septemba 1976) alikuwa kiongozi wa Chama cha kikomunisti cha China tangu 1935 hadi kifo chake na kiongozi mkuu wa China tangu 1949.
Aliongoza wakomunisti katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya China dhidi ya serikali ya Kuomintang na dhidi ya jeshi la Japan wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.
Mao alibadilisha itikadi ya Umarx-Ulenin kwa mahitaji ya wakomunisti wa China. Mwelekeo wake huitwa "Umao". Alijaribu kujenga ukomunisti nchini kwa kutegemea wakulima kuliko wanafayakazi jinsi ilivyokuwa itikadi ya kawaida ya Ukomunisti.
Siasa yake ya kiuchumi ilisababisha njaa na vifo vingi. Dhidi ya wapinzani wake ndani ya chama alianzisha tangu 1966 "mapinduzi ya kiutamaduni" iliyoharibu mapokeo mengi na sehemu kubwa ya urithi wa kihistoria ya China. Kwa jumla ni watu milioni 35 hadi 70 wanaokadiriwa walikufa kutokana na njaa au mateso chini ya Mao.