Tallinn
From Wikipedia
Tallinn ni mji mkuu na pia mji mkubwa wa Estonia mwenye wakazi 400,000. Iko mwambaoni wa Ghuba ya Ufini ya Baltiki na bandari yake ni bandari kuu ya nchi.
Tallinn inajulikana kwa mji wa kale ulioingizwa na UNESCO kastika orodha la urithi wa dunia.
Historia yake ni ya karne nyingi. Kwa Zama za Kati ilikuwa mji mwanachama wa shirikisho la Hanse ijatajirika kutukana na biashara kati ya Urusi, Skandinavia na Ujerumani.
Tangu 1918 Tallinn imekuwa mji mkuu wa Estonia huria.
1940 mji pamoja na nchi yote vilivamiwa na jeshi la Kisovyeti ikawa mji mkuu wa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiestonia hadi 1991 halafu tena mji mkuu wa Estonia huria.