Amerika ya Kusini
From Wikipedia
Amerika ya Kusini ni bara upande wa Kusini mwa Ikweta. Inapakana na Bahari ya Pasifiki upande wa Magharibi, na Bahari ya Atlantiki upande wa Mashariki.
Katika bara hilo kuna nchi zifuatazo:
- Argentina
- Bolivia
- Brazil
- Chile
- Ekuador
- Guyana
- Guyana ya Kifaransa
- Kolombia
- Paraguay
- Peru
- Surinam
- Uruguay
- Venezuela
[edit] Urithi wa ukoloni: Lugha na utamaduni
Kwa lugha mablimbali bara inahesabiwa katika "Amerika ya Kilatini" kwa sababu wakazi wengi hutumia lugha za Kirumi hasa Kihispania na Kireno zilizizotokana na Kilatini.
Sababu yake ni ya kwamba sehemu kubwa ya bara hii ilikuwa koloni ya Hispania. Brazil ilikuwa koloni ya Ureno. Nchi zote mbili ziliacha tabia za utamaduni wao pamoja na lugha zilizokuwa lugha za kitaifa.
Nchi za Guyana pekee zilikuwa koloni za mataifa mengine ya Ulaya zilizoacha lugha zao:
- Guyana ilikuwa koloni ya Uingereza ikitumia Kiingereza (zamani illitwa Guyana ya Kiingereza)
- Surinam ilikuwa koloni ya Uholanzi ikitumia Kiholanzi (zamani illitwa Guyana ya Kiholanzi)
- Guyana ya Kifaransa ilikuwa koloni ya Ufaransa imekuwa mkoa wa Ufaransa na sehemu ya Umoja wa Ulaya ikitumia Kifaransa.
Categories: Mbegu | Bara | Amerika Kusini | Amerika